Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 3:1-15 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Wafuatao ndio wazawa wa Aroni na Mose wakati Mwenyezi-Mungu alipozungumza na Mose mlimani Sinai.

2. Haya ndiyo majina ya wana wa Aroni: Nadabu, mzaliwa wake wa kwanza, Abihu, Eleazari na Ithamari.

3. Hawa waliwekwa wakfu kwa kupakwa mafuta wawe makuhani.

4. Lakini Nadabu na Abihu walikufa mbele ya Mwenyezi-Mungu, wakati walipomtolea Mwenyezi-Mungu moto usio mtakatifu katika jangwa la Sinai. Wao hawakuwa na watoto kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakawa wanahudumu kama makuhani wakati wa uhai wa Aroni baba yao.

5. Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose,

6. “Walete karibu watu wa kabila la Lawi, uwaweke mbele ya kuhani Aroni ili uwape jukumu la kumtumikia.

7. Watafanya kazi kwa niaba yake na ya jumuiya yote kwenye hema la mkutano wanapohudumu mahali patakatifu,

8. wataangalia na kutunza vyombo vyote vya hema la mkutano na kuwasaidia Waisraeli wanapotoa huduma zao kwenye mahali patakatifu.

9. Walawi utampa Aroni na wazawa wake makuhani; hao wametolewa kati ya Waisraeli wawahudumie kabisa.

10. Utawateua Aroni na wanawe ili waweze kutekeleza huduma zao za ukuhani; lakini kama mtu yeyote mwingine atakaribia, atauawa.”

11. Mwenyezi-Mungu akaendelea kumwambia Mose,

12. “Angalia, sasa nimewateua Walawi miongoni mwa Waisraeli wote, badala ya kila mzaliwa wa kwanza wa kiume kifunguamimba katika kila familia ya Israeli. Walawi ni wangu,

13. kwani kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli ni wangu. Wakati nilipowaua wazaliwa wa kwanza wote wa Wamisri nilijiwekea wakfu kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli; kila mzaliwa wa kwanza wa binadamu hata wa mnyama; wao watakuwa wangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.”

14. Baadaye Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose katika jangwa la Sinai,

15. “Wahesabu wana wa Lawi wote kulingana na koo zao na familia zao, kila mwanamume kuanzia watoto wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi.”

Kusoma sura kamili Hesabu 3