Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 27:9-15 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Ikiwa hana binti, basi urithi huo watapewa ndugu zake wa kiume.

10. Na ikiwa hana ndugu wa kiume, basi urithi wake utawaendea baba zake, wakubwa na wadogo.

11. Na ikiwa baba yake hana ndugu wa kiume, basi urithi wake utakuwa wa jamaa yake wa karibu, naye ataumiliki kama mali yake. Hii itakuwa kanuni na sheria kwa Waisraeli, kama vile mimi Mwenyezi-Mungu nilivyokuamuru.”

12. Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Panda juu ya Mlima huu wa miinuko ya Abarimu uitazame nchi ambayo nimewapa Waisraeli.

13. Ukisha iona, nawe pia utafariki kama ndugu yako Aroni alivyofariki,

14. kwa sababu hamkuitii amri yangu kule jangwani Sini. Wakati jumuiya yote ya watu walipolalamika juu yangu kule Meriba, hamkuacha utukufu wangu uonekane mbele yao walipotaka wapewe maji.” (Meriba ni chemchemi ya maji ya Kadeshi katika jangwa la Sini).

15. Naye Mose akamwomba Mwenyezi-Mungu,

Kusoma sura kamili Hesabu 27