Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 26:51-61 Biblia Habari Njema (BHN)

51. Idadi ya wanaume Waisraeli waliohesabiwa ilikuwa 601,730.

52. Kisha Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose,

53. “Makabila haya yatagawiwa nchi iwe urithi wao, kulingana na idadi ya majina yao.

54. Kabila kubwa litapewa sehemu yao kubwa na dogo litapewa sehemu yao ndogo. Kila kabila litapewa urithi wake kulingana na idadi ya watu wake.

55. Hata hivyo ugawaji wa nchi utafanywa kwa kura. Kila kabila litarithi kulingana na majina ya ukoo wao.

56. Urithi wa kila kabila utagawanywa kwa kura, kila kabila litapata kulingana na ukubwa au udogo wake.”

57. Hizi ndizo koo za Walawi zilizoorodheshwa na jamaa zao: Gershoni, Kohathi na Merari,

58. Pamoja na jamaa za Libni, Hebroni, Mahli, Mushi na Kora. Kohathi alikuwa baba yake Amramu.

59. Mkewe Amramu aliitwa Yokebedi binti yake Lawi, aliyezaliwa Misri. Huyu alimzalia Amramu watoto wawili wa kiume, Aroni na Mose, na binti mmoja, Miriamu.

60. Aroni alikuwa na watoto wa kiume wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

61. Nadabu na Abihu walikufa walipomtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya moto usiofaa.

Kusoma sura kamili Hesabu 26