Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 26:5-25 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Kwanza ni kabila la Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo. Henoki, Palu,

6. Hesroni na Karmi.

7. Hizo ndizo koo za kabila la Reubeni. Idadi ya wanaume waliohesabiwa ni 43,730.

8. Wazawa wa Palu walikuwa Eliabu,

9. na wanawe Nemueli, Dathani na Abiramu. (Hawa wawili: Dathani na Abiramu, ndio waliokuwa wamechaguliwa miongoni mwa jumuiya, lakini wakampinga Mose na Aroni, na kujiunga na wafuasi wa Kora wakati walipomwasi Mwenyezi-Mungu.

10. Wakati huo ardhi ilifunguka ikawameza, wakafa pamoja na Kora na wafuasi wake moto ulipoangamiza watu 250; wakawa onyo kwa watu.

11. Pamoja na hayo wana wa Kora hawakufa.)

12. Kabila la Simeoni. Nemueli, Yamini, Yakini,

13. Zera na Shauli.

14. Hizo ndizo koo za kabila la Simeoni, jumla yao wanaume 22,000.

15. Kabila la Gadi lilikuwa na jamaa za Sefoni, Hagi, Shuni,

16. Ozni, Eri,

17. Arodi na Areli.

18. Hizo ndizo koo za kabila la Gadi, jumla wanaume 40,500.

19. Kabila la Yuda lilikuwa na wanawe wa Yuda Eri na Onani. Hawa walifia nchini Kanaani.

20. Kabila la Yuda lilikuwa na jamaa za Shela, Peresi, na Zera.

21. Kutoka kwa Peresi, familia ya Hesroni na Hamuli.

22. Hizo ndizo koo za Yuda, jumla wanaume 76,500.

23. Kabila la Isakari lilikuwa na jamaa za Tola, Puva,

24. Yashubu na wa Shimroni.

25. Hizo ndizo koo za Isakari, jumla wanaume 64,300.

Kusoma sura kamili Hesabu 26