Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 26:36-51 Biblia Habari Njema (BHN)

36. Ukoo wa Erani ulikuwa na jamaa ya Shuthela.

37. Hizo ndizo koo za Efraimu, jumla wanaume 32,500. Zote hizo zilitokana na Yosefu.

38. Kabila la Benyamini lilikuwa na jamaa za Bela, Ashbeli, Ahiramu,

39. Shufamu na Hufamu.

40. Koo za Ardi na Naamani, zilitokana na Bela.

41. Hizo ndizo koo za Benyamini, jumla wanaume 45,600.

42. Kabila la Dani lilikuwa na jamaa ya Shuhamu;

43. ukoo ulikuwa na wanaume 64,400.

44. Kabila la Asheri lilikuwa na jamaa za Imna, Ishvi na Beria.

45. Koo za Heberi na Malkieli zilitokana na Beria.

46. Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera.

47. Hizo ndizo koo za kabila la Asheri, jumla wanaume 53,400.

48. Kabila la Naftali lilikuwa na jamaa za Yaseeli, Guni,

49. Yeseri na Shilemu.

50. Hizi ndizo koo za kabila la Naftali, jumla wanaume 45,400.

51. Idadi ya wanaume Waisraeli waliohesabiwa ilikuwa 601,730.

Kusoma sura kamili Hesabu 26