Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 24:7-15 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Watakuwa na hazina ya kutosha ya maji,mbegu yao itapata maji mengi,mfalme wao atakuwa mkuu kuliko Agagi,na ufalme wake utatukuka sana.

8. Mungu aliwachukua kutoka Misri,naye huwapigania kwa nguvu kama nyati.Atayateketeza mataifa yaliyo adui zao,atavunjavunja mifupa yao,atawachoma kwa mishale yake.

9. Ataotea na kulala chini kama simba,nani atathubutu kumwamsha?Abarikiwe yeyote atakayewabariki nyinyi Waisraeli,alaaniwe yeyote atakayewalaani.

10. Balaki akawaka hasira dhidi ya Balaamu, akakunja mikono kwa ghadhabu na kumwambia, “Nilikuita uwalaani adui zangu, lakini mara hizi zote tatu umewabariki!

11. Sasa! Nenda zako. Nilikuwa nimekuahidi kukupa zawadi nyingi, lakini Mwenyezi-Mungu hakukujalia kupata zawadi hizo, amekunyima!”

12. Balaamu akamjibu Balaki, “Je, sikuwaambia wajumbe uliowatuma kwangu

13. kwamba hata kama ungenipa nyumba yako imejaa fedha na dhahabu, mimi sitaweza kukiuka agizo la Mwenyezi-Mungu, kwa kufanya jambo lolote, jema au baya kwa hiari yangu mwenyewe? Nilisema, atakachosema Mwenyezi-Mungu ndicho nitakachokisema.

14. “Sasa ninarudi kwa watu wangu, lakini kabla sijaondoka, acha nikuambie mambo ambayo watu hao watawatendea watu wako siku zijazo.”

15. Basi, Balaamu akatamka kauli hii:“Kauli yangu mimi Balaamu mwana wa Beori,kauli ya mtu aliyefumbuliwa macho,

Kusoma sura kamili Hesabu 24