Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 24:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Sasa Balaamu alitambua kwamba Mwenyezi-Mungu alipenda kuwabariki Waisraeli, kwa hiyo hakwenda kupiga bao tena, akawa anaangalia jangwani.

2. Alitazama juu akawaona Waisraeli wamepiga kambi, kila kabila mahali pake. Kisha roho ya Mungu ikamjia,

3. naye akatamka kauli hii ya kinabii:Kauli yangu mimi Balaamu mwana wa Peorikauli ya mtu aliyefumbuliwa macho;

4. kauli ya mtu aliyesikia maneno ya Mungumtu aliyeona maono ya Mungu Mwenye Nguvu,mtu anayesujudu na kuona wazi.

Kusoma sura kamili Hesabu 24