Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 21:25-35 Biblia Habari Njema (BHN)

25. Waisraeli waliiteka miji hii yote nao wakaishi katika miji ya Waamori katika Heshboni na vitongoji vyake.

26. Heshboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye hapo awali alikuwa amepigana na mfalme wa Moabu na kuiteka nchi yake yote mpaka mto Arnoni.

27. Ndiyo maana washairi wetu huimba:“Njoni Heshboni na kujenga.Mji wa Sihoni na ujengwe na kuimarishwa.

28. Maana moto ulitoka Heshboni,miali ya moto ilitoka mjini kwa Sihoni,uliuteketeza mji wa Ari wa Moabu,ukaiangamiza milima ya mto Arnoni.

29. Ole wenu watu wa Moabu!Mmeangamizwa, enyi watu wa mungu Kemoshi!Umewafanya watoto wenu wa kiume kuwa wakimbizi,binti zako umewaacha wachukuliwe matekampaka kwa Sihoni, mfalme wa Amori.

30. Lakini sasa wazawa wao wameangamizwa,kutoka Heshboni mpaka Diboni,kutoka Nashimu mpaka Nofa, karibu na Medeba.”

31. Basi, Waisraeli wakakaa katika nchi ya Waamori.

32. Kisha Mose alituma watu wapeleleze mji wa Yazeri; wakauteka pamoja na vitongoji vyake, wakawafukuza Waamori waliokaa humo.

33. Waisraeli waligeuka wakafuata njia iendayo Bashani. Mfalme Ogu wa Bashani akatoka na jeshi lake kuwashambulia huko Edrei.

34. Lakini Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Usimwogope, maana nimemtia mikononi mwako pamoja na watu wake wote na nchi yake yote. Utamtendea kama ulivyomtendea Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekuwa anakaa Heshboni.”

35. Basi, Waisraeli wakamuua Ogu, wanawe na watu wake wote, bila kumwacha hata mtu mmoja, kisha wakaitwaa nchi yake.

Kusoma sura kamili Hesabu 21