Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 21:19-28 Biblia Habari Njema (BHN)

19. kutoka Matana mpaka Nahalieli, kutoka Nahalieli mpaka Bamothi,

20. na kutoka Bamothi mpaka kwenye bonde linaloingia nchi ya Moabu, kwenye kilele cha Mlima Pisga, kielekeacho chini jangwani.

21. Waisraeli walimpelekea mfalme Sihoni wa Waamori, ujumbe huu:

22. “Turuhusu tupite katika nchi yako; hatutakwenda pembeni na kuingia mashambani au katika mashamba ya mizabibu, wala hatutakunywa maji ya visima vyenu; tutapita moja kwa moja katika barabara kuu ya mfalme mpaka tumeondoka nchini mwako.”

23. Lakini Sihoni hakuwaruhusu watu wa Israeli wapite katika nchi yake. Aliwakusanya watu wake, akaenda Yahasa Jangwani kuwashambulia Waisraeli.

24. Lakini Waisraeli walimuua, wakaitwaa nchi yake tangu mto Arnoni hadi mto Yaboki, yaani hadi mpaka wa nchi ya Waamoni ambao ulikuwa unalindwa sana.

25. Waisraeli waliiteka miji hii yote nao wakaishi katika miji ya Waamori katika Heshboni na vitongoji vyake.

26. Heshboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye hapo awali alikuwa amepigana na mfalme wa Moabu na kuiteka nchi yake yote mpaka mto Arnoni.

27. Ndiyo maana washairi wetu huimba:“Njoni Heshboni na kujenga.Mji wa Sihoni na ujengwe na kuimarishwa.

28. Maana moto ulitoka Heshboni,miali ya moto ilitoka mjini kwa Sihoni,uliuteketeza mji wa Ari wa Moabu,ukaiangamiza milima ya mto Arnoni.

Kusoma sura kamili Hesabu 21