Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 21:16-25 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Kutoka huko Waisraeli walisafiri mpaka Beeri; yaani kisima ambapo Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, “Wakusanyeni watu pamoja, nami nitawapa maji.”

17. Hapo Waisraeli waliimba wimbo huu:“Bubujika maji ee kisima! – Kiimbieni!

18. Kisima kilichochimbwa na wakuukilichochimbwa sana na wenye cheo,kwa fimbo zao za enzi na bakora.”Kutoka jangwani walisafiri mpaka Matana,

19. kutoka Matana mpaka Nahalieli, kutoka Nahalieli mpaka Bamothi,

20. na kutoka Bamothi mpaka kwenye bonde linaloingia nchi ya Moabu, kwenye kilele cha Mlima Pisga, kielekeacho chini jangwani.

21. Waisraeli walimpelekea mfalme Sihoni wa Waamori, ujumbe huu:

22. “Turuhusu tupite katika nchi yako; hatutakwenda pembeni na kuingia mashambani au katika mashamba ya mizabibu, wala hatutakunywa maji ya visima vyenu; tutapita moja kwa moja katika barabara kuu ya mfalme mpaka tumeondoka nchini mwako.”

23. Lakini Sihoni hakuwaruhusu watu wa Israeli wapite katika nchi yake. Aliwakusanya watu wake, akaenda Yahasa Jangwani kuwashambulia Waisraeli.

24. Lakini Waisraeli walimuua, wakaitwaa nchi yake tangu mto Arnoni hadi mto Yaboki, yaani hadi mpaka wa nchi ya Waamoni ambao ulikuwa unalindwa sana.

25. Waisraeli waliiteka miji hii yote nao wakaishi katika miji ya Waamori katika Heshboni na vitongoji vyake.

Kusoma sura kamili Hesabu 21