Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 1:48-54 Biblia Habari Njema (BHN)

48. kwa sababu Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose,

49. “Usihesabu kabila la Lawi wala usiwafanyie sensa kati ya watu wa Israeli;

50. bali utawateua wawe waangalizi wa hema la ushuhuda, vyombo vyake vyote na kila kitu kilichomo ndani yake; watakuwa wakilibeba pamoja na vyombo vyake vyote. Watahudumu humo ndani na kupiga kambi yao kwa kulizunguka.

51. Tena wakati wa hema kungolewa Walawi ndio watakaolingoa na wakati wa hema kusimikwa Walawi ndio watakaolisimamisha.

52. Waisraeli wengine wote watapiga kambi zao makundimakundi, kila mtu katika kundi lake na chini ya bendera yake.

53. Lakini Walawi watapiga kambi zao kulizunguka hema la maamuzi, wakililinda ili mtu yeyote asije akalikaribia na kusababisha ghadhabu yangu kuwaka dhidi ya jumuiya ya watu wa Israeli; basi Walawi watalitunza hema la maamuzi.”

54. Kwa hiyo Waisraeli wakafanya kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Kusoma sura kamili Hesabu 1