Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 1:41-50 Biblia Habari Njema (BHN)

41. walikuwa watu 41,500.

42. Kutoka kabila la Naftali, kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina ya mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini,

43. walikuwa watu 53,400.

44. Hawa ndio watu waliokuwa wamehesabiwa ambao Mose na Aroni waliwahesabu wakisaidiwa na wale viongozi kumi na wawili wa Israeli, kila kiongozi akiwakilisha ukoo wake.

45. Hivyo jumla ya wanaume wote wa Israeli wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini nchini Israeli

46. ilikuwa watu 603,550.

47. Lakini Walawi hawakuhesabiwa pamoja na yale makabila mengine,

48. kwa sababu Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose,

49. “Usihesabu kabila la Lawi wala usiwafanyie sensa kati ya watu wa Israeli;

50. bali utawateua wawe waangalizi wa hema la ushuhuda, vyombo vyake vyote na kila kitu kilichomo ndani yake; watakuwa wakilibeba pamoja na vyombo vyake vyote. Watahudumu humo ndani na kupiga kambi yao kwa kulizunguka.

Kusoma sura kamili Hesabu 1