Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 1:26-36 Biblia Habari Njema (BHN)

26. Kutoka kabila la Yuda kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini,

27. walikuwa watu 74,600.

28. Kutoka kabila la Isakari kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini,

29. walikuwa watu 54,400.

30. Kutoka kabila la Zebuluni kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini,

31. walikuwa watu 57,400.

32. Kutoka kabila la Efraimu, mwanawe Yosefu, kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini,

33. walikuwa watu 40,500.

34. Kutoka kabila la Manase, mwanawe Yosefu, kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi waliofaa kuingia jeshini,

35. walikuwa watu 32,200.

36. Kutoka kabila la Benyamini, kwa kufuata vizazi vyao kulingana na familia zao na jamaa zao kadiri ya jumla ya majina yao mmojammoja, wenye umri kuanzia miaka ishirini na zaidi, waliofaa kuingia jeshini,

Kusoma sura kamili Hesabu 1