Agano la Kale

Agano Jipya

Habakuki 2:7-11 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Siku moja wadeni wako watainuka ghafla,wale wanaokutetemesha wataamka.Ndipo utakuwa mateka wao.

8. Wewe umeyapora mataifa mengi,lakini wote wanaosalimika watakupora wewe,kwa mauaji na dhuluma uliyoitendea dunia,naam, uliyoifanyia miji na wakazi wake wote.

9. “Ole wako unayejitajirisha kwa hasara ya mwingine,ujengaye nyumba yako juu milimaniukidhani kuwa salama mbali na madhara.

10. Lakini kwa mipango yako umeiaibisha jamaa yako.Kwa kuyaangamiza mataifa mengi,umeyaangamiza maisha yako mwenyewe.

11. Ndiyo maana hata mawe yatalalamika ukutani,na boriti za nyumba zitayaunga mkono.

Kusoma sura kamili Habakuki 2