Agano la Kale

Agano Jipya

Habakuki 2:6-16 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Kila mtu atamdhihaki mtu wa namna hiyona kumtungia misemo ya dhihaka:“Ole wako unayejirundikia visivyo vyako,na kuchukua rehani mali za watu lakini hulipi!Utaendelea kufanya hivyo hadi lini?

7. Siku moja wadeni wako watainuka ghafla,wale wanaokutetemesha wataamka.Ndipo utakuwa mateka wao.

8. Wewe umeyapora mataifa mengi,lakini wote wanaosalimika watakupora wewe,kwa mauaji na dhuluma uliyoitendea dunia,naam, uliyoifanyia miji na wakazi wake wote.

9. “Ole wako unayejitajirisha kwa hasara ya mwingine,ujengaye nyumba yako juu milimaniukidhani kuwa salama mbali na madhara.

10. Lakini kwa mipango yako umeiaibisha jamaa yako.Kwa kuyaangamiza mataifa mengi,umeyaangamiza maisha yako mwenyewe.

11. Ndiyo maana hata mawe yatalalamika ukutani,na boriti za nyumba zitayaunga mkono.

12. “Ole wako unayejenga mji kwa mauajiunayesimika jiji kwa maovu!

13. Mwenyezi-Mungu wa majeshi husababishajuhudi za watu zipotelee motoni,na mataifa yajishughulishe bure.

14. Utukufu wa Mwenyezi-Mungu utaenea pote duniani,kama vile maji yaeneavyo baharini.

15. Ole wako unayewalewesha jirani zako,na kutia sumu katika divai yaoili upate kuwaona wamekaa uchi.

16. Utajaa aibu badala ya heshima.Utakunywa wewe mwenyewe na kupepesuka!Mwenyezi-Mungu mwenyewe atakulevya,na aibu itaifunika heshima yako!

Kusoma sura kamili Habakuki 2