Agano la Kale

Agano Jipya

Habakuki 2:16-18 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Utajaa aibu badala ya heshima.Utakunywa wewe mwenyewe na kupepesuka!Mwenyezi-Mungu mwenyewe atakulevya,na aibu itaifunika heshima yako!

17. Maovu uliyoitenda Lebanoni yatakuvamia wewe;uliwaua wanyama, wanyama nao watakutisha.Yote hayo yatakupata wewe,kwa mauaji na dhuluma uliyoitendea dunia,naam, uliyoifanyia miji na wakazi wake wote.

18. “Chafaa nini kinyago alichotengeneza mtu?Sanamu ni madini yaliyoyeyushwa,ni kitu cha kueneza udanganyifu!Mtengeneza sanamu hutumaini alichotengeneza mwenyewe,kinyago ambacho hakiwezi hata kusema!

Kusoma sura kamili Habakuki 2