Agano la Kale

Agano Jipya

Habakuki 2:12-16 Biblia Habari Njema (BHN)

12. “Ole wako unayejenga mji kwa mauajiunayesimika jiji kwa maovu!

13. Mwenyezi-Mungu wa majeshi husababishajuhudi za watu zipotelee motoni,na mataifa yajishughulishe bure.

14. Utukufu wa Mwenyezi-Mungu utaenea pote duniani,kama vile maji yaeneavyo baharini.

15. Ole wako unayewalewesha jirani zako,na kutia sumu katika divai yaoili upate kuwaona wamekaa uchi.

16. Utajaa aibu badala ya heshima.Utakunywa wewe mwenyewe na kupepesuka!Mwenyezi-Mungu mwenyewe atakulevya,na aibu itaifunika heshima yako!

Kusoma sura kamili Habakuki 2