Agano la Kale

Agano Jipya

Habakuki 2:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mimi nitasimama mahali pa kuchungulia,na kukaa juu mnarani;nitakaa macho nione ataniambia nini,atajibu nini kuhusu lalamiko langu.”

2. Kisha, Mwenyezi-Mungu akanijibu hivi:“Yaandike maono haya;yaandike wazi juu ya vibao,anayepitia hapo apate kuyasoma.

3. Maono haya yanangoja wakati wa kufaa;ni maono ya ukweli juu ya mwisho.Kama yaonekana kuchelewa, uyasubiri;hakika yatafika, wala hayatachelewa.

Kusoma sura kamili Habakuki 2