Agano la Kale

Agano Jipya

Habakuki 1:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kauli ya Mungu aliyoiona nabii Habakuki.

2. “Ee Mwenyezi-Mungu, nitakulilia mpaka lini,nawe usinisikilize na kunisaidia?Kwa nini nalia: ‘Dhuluma’nawe hutuokoi?

3. Kwa nini wanifanya nishuhudie mabaya na taabu?Uharibifu na ukatili vinanizunguka,ugomvi na mashindano yanazuka.

4. Hivyo sheria haina nguvu,wala haki haitekelezwi.Waovu wanawazunguka waadilifu,hivyo hukumu hutolewa ikiwa imepotoshwa.”

5. Mungu akasema:“Yaangalie mataifa, uone!Utastaajabu na kushangaa.Maana ninatenda kitu ukiwa bado unaishi,kitu ambacho ungeambiwa hungesadiki.

6. Maana ninawachochea Wakaldayo,taifa lile kali na lenye hamaki!Taifa lipitalo katika nchi yote,ili kunyakua makao ya watu wengine.

7. Wao ni watu wa kuchukiza na kutisha;wao hujiamulia wenyewe nini haki na adhama.

8. “Farasi wao ni wepesi kuliko chui;wakali kuliko mbwamwitu wenye njaa.Wapandafarasi wao wanatoka mbali,wanaruka kasi kama tai arukiavyo mawindo.

Kusoma sura kamili Habakuki 1