Agano la Kale

Agano Jipya

Ezra 8:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ifuatayo ni orodha ya viongozi wa koo za watu waliorudi pamoja nami Ezra kutoka Babuloni, wakati wa utawala wa mfalme Artashasta:

2. Gershomu, wa ukoo wa Finehasi. Danieli, wa ukoo wa Ithamari. Hatushi, wa ukoo wa Daudi,

3. aliyekuwa mwana wa Shekania. Zekaria, wa ukoo wa Paroshi, pamoja na wanaume 150 wa ukoo wake, walioandikishwa pamoja.

4. Eliehoenai, mwana wa Zerahia, wa ukoo wa Pahath-moabu, pamoja na wanaume 200.

5. Shekania, mwana wa Yahazieli, wa ukoo wa Zatu, pamoja na wanaume 300.

6. Ebedi, mwana wa Yonathani, wa ukoo wa Adini, pamoja na wanaume 50.

7. Yeshaya, mwana wa Athalia, wa ukoo wa Elamu, pamoja na wanaume 70.

8. Zebadia, mwana wa Mikaeli, wa ukoo wa Shefatia, pamoja na wanaume 80.

Kusoma sura kamili Ezra 8