Agano la Kale

Agano Jipya

Ezra 2:49-63 Biblia Habari Njema (BHN)

49. ukoo wa Uza, wa Pasea, wa Besai,

50. ukoo wa Asna, wa Meunimu, wa Nefisimu,

51. ukoo wa Bakbuki, wa Hakufa, wa Harhuri,

52. ukoo wa Basluthi, wa Mehida, wa Harsha,

53. ukoo wa Barkosi, wa Sisera, wa Tema,

54. ukoo wa Nezia na wa Hatifa.

55. Koo za wazawa wa watumishi wa Solomoni waliorudi kutoka uhamishoni zilikuwa, ukoo wa Sotai, wa Hasoferethi, wa Perudha,

56. ukoo wa Yaala, wa Darkoni, wa Gideli,

57. ukoo wa Shefatia, wa Hatili, wa Pokereth-hasebaimu na wa Ami.

58. Nao watumishi wote wa hekalu na wazawa wa watumishi wa Solomoni waliorudi kutoka uhamishoni walikuwa watu 392.

59. Watu wa miji ifuatayo, pia walirudi: Wa mji wa Tel-mela, wa Tel-harsha, wa Kerubu, wa Adani na wa Imeri, ila hawakuweza kuthibitisha kuwa walikuwa wazawa wa Waisraeli.

60. Wao walikuwa watu wa ukoo wa Delaya wa Tobia na wa Nekoda, jumla watu 652.

61. Watu wa koo zifuatazo za makuhani pia walirudi: Ukoo wa Habaya, wa Hakosi na wa Barzilai. Huyo Barzilai alikuwa ameoa binti Barzilai wa Gileadi, naye pia akaitwa Barzilai.

62. Hao walitafuta orodha yao katika kumbukumbu za koo, lakini hawakuonekana humo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kushika ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi.

63. Mtawala akawaambia kuwa hawaruhusiwi kushiriki chakula kitakatifu sana, mpaka awepo kuhani atakayeweza kutoa kauli ya Urimu na Thumimu.

Kusoma sura kamili Ezra 2