Agano la Kale

Agano Jipya

Ezra 1:7-11 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Mfalme Koreshi aliwarudishia vyombo ambavyo mfalme Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kuviweka katika nyumba ya miungu yake.

8. Alimkabidhi Mithredathi, mtunza hazina, vyombo hivyo, naye akamhesabia Sheshbaza, mtawala wa Yuda.

9. Ifuatayo ndiyo hesabu yake:Bakuli 30 za dhahabu;bakuli 1,000 za fedha;vyetezo 29;

10. bakuli ndogo za dhahabu 30;bakuli ndogo za fedha 410;vyombo vinginevyo 1,000.

11. Vyombo vyote vya dhahabu na fedha, pamoja na vitu vinginevyo vilikuwa jumla yake 5,400. Vyote hivi, Sheshbaza alivichukua hadi Yerusalemu wakati yeye pamoja na watu wengine alipotolewa uhamishoni Babuloni kwenda Yerusalemu.

Kusoma sura kamili Ezra 1