Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 7:6-16 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Mwisho umekuja!Naam, mwisho umefika!Umewafikia nyinyi!

7. Enyi wakazi wa nchi hii, maangamizi yenu yamewajia!Wakati umekuja;naam, siku imekaribia.Hiyo ni siku ya msukosukona siyo ya sauti za shangwe mlimani.

8. Sasa mtausikia uzito wa hasira yangu juu yenu.Nitawahukumu kulingana na mwenendo wenu;nitawaadhibu kadiri ya machukizo yenu.

9. Sitawaachilia wala sitawaonea huruma.Nitawaadhibu kulingana na mienendo yenumaadamu machukizo yapo bado miongoni mwenu.Ndipo mtakapotambua kuwa ni mimi Mwenyezi-Mungu ninayewaangamiza.

10. “Tazameni, siku ile inakuja!Maangamizi yenu yamekuja.Ukatili uko kila mahali na kiburi kimechanua.

11. Ukatili unaendelea kuwa mbaya zaidi.Hakuna hata mmoja wenu atakayebaki,wala vitu mlivyojirundikia kwa wingi au utajiri wenu;hatakuwako mtu mwenye heshima miongoni mwenu.

12. Wakati umewadia,naam, ile siku imekaribia.Mnunuzi asifurahi wala mwuzaji asiomboleze;kwa sababu ghadhabu yangu itaukumba umati wote.

13. Wauzaji hawataweza kurudia mali yao waliyouzahata kama wakibaki hai.Kwani maono haya yahusu umati wote na hayatabatilishwa.Kutokana na uovu huo, hakuna mtu atakayesalimisha maisha yake.

14. Tarumbeta imepigwa na kuwafanya wote wawe tayari.Lakini hakuna anayekwenda vitani,kwani ghadhabu yangu iko juu ya umati wote.

15. Nje kuna kifo kwa upangana ndani ya mji kuna maradhi mabaya na njaa.Walioko shambani watakufa kwa upanga;walio mjini njaa na maradhi mabaya yatawaangamiza.

16. Wakiwapo watu watakaosalimikawatakimbilia milimani kama hua waliotishwa bondeni.Kila mmoja wao ataomboleza kwa dhambi zake.

Kusoma sura kamili Ezekieli 7