Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 7:2-10 Biblia Habari Njema (BHN)

2. “Wewe mtu, waambie wakazi wa nchi ya Israeli kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Sasa ni mwisho!Mwisho umeifikia nchi yote kutoka pande zote nne!

3. Sasa mwisho umewafikia;sasa mtausikia ukali wa hasira yangu juu yenu.Nitawahukumu kadiri ya mwenendo wenu.Nitawaadhibu kwa machukizo yenu yote.

4. Sitawaachia wala sitawahurumia;nitawaadhibu kulingana na mienendo yenu,maadamu machukizo bado yapo kati yenu.Ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.

5. Ninachosema mimi Bwana Mwenyezi-Mungu ni hiki:Mtapatwa na maafa mfululizo!

6. Mwisho umekuja!Naam, mwisho umefika!Umewafikia nyinyi!

7. Enyi wakazi wa nchi hii, maangamizi yenu yamewajia!Wakati umekuja;naam, siku imekaribia.Hiyo ni siku ya msukosukona siyo ya sauti za shangwe mlimani.

8. Sasa mtausikia uzito wa hasira yangu juu yenu.Nitawahukumu kulingana na mwenendo wenu;nitawaadhibu kadiri ya machukizo yenu.

9. Sitawaachilia wala sitawaonea huruma.Nitawaadhibu kulingana na mienendo yenumaadamu machukizo yapo bado miongoni mwenu.Ndipo mtakapotambua kuwa ni mimi Mwenyezi-Mungu ninayewaangamiza.

10. “Tazameni, siku ile inakuja!Maangamizi yenu yamekuja.Ukatili uko kila mahali na kiburi kimechanua.

Kusoma sura kamili Ezekieli 7