Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 5:2-5 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Baada ya kuzingirwa kwa mji wa Yerusalemu kumalizika, utaichoma theluthi ya nywele zako ndani ya mji. Theluthi nyingine utaipigapiga kwa upanga ukiuzunguka mji. Theluthi ya mwisho utaitawanya kwa upepo, nami nitauchomoa upanga wangu ili kuifuatilia.

3. Sehemu ndogo tu ya nywele zako utaichukua na kuifunga kwenye mkunjo wa joho lako.

4. Lakini chukua pia nywele kidogo uzitupe motoni na kuziteketeza. Moto utatokea humo na kuwaunguza watu wote wa Israeli.

5. “Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Ndivyo itakavyokuwa kuhusu mji wa Yerusalemu. Mimi niliuweka kuwa katikati ya mataifa, umezungukwa na nchi za kigeni pande zote.

Kusoma sura kamili Ezekieli 5