Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 36:6-11 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Kwa hiyo, ewe mtu, toa unabii kuhusu nchi ya Israeli, uiambie milima na vilima, vijito na mabonde kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema mambo haya kutokana na ghadhabu yangu yenye wivu juu ya nchi yangu, kwa sababu imetukanwa na watu wa mataifa.

7. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Ninaapa kwamba watu wa mataifa yaliyo jirani nanyi watatukanwa wao wenyewe.

8. “Lakini kuhusu milima ya Israeli, miti itatoa matawi na kuzaa matunda kwa ajili ya watu wangu wa Israeli, maana wao watarudi makwao karibuni.

9. Mimi niko upande wenu, nitahakikisha kuwa mnalimwa na kupandwa mbegu.

10. Waisraeli nitawazidisha sana. Miji itakaliwa, na magofu yatajengwa upya.

11. Nitawafanya watu na wanyama waongezeke na kuwa wengi. Nitawafanya nyinyi milima mkaliwe tena kama zamani. Nitawatendea mema mengi kuliko zamani. Nanyi mtatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.

Kusoma sura kamili Ezekieli 36