Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 36:5-10 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Sasa kwa kuwa mimi nimechukizwa mno, nitayaadhibu mataifa mengine na hasa watu wa Edomu. Wao kwa furaha moyoni na madharau waliichukua hiyo nchi iliyo yangu iwe yao.

6. Kwa hiyo, ewe mtu, toa unabii kuhusu nchi ya Israeli, uiambie milima na vilima, vijito na mabonde kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema mambo haya kutokana na ghadhabu yangu yenye wivu juu ya nchi yangu, kwa sababu imetukanwa na watu wa mataifa.

7. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Ninaapa kwamba watu wa mataifa yaliyo jirani nanyi watatukanwa wao wenyewe.

8. “Lakini kuhusu milima ya Israeli, miti itatoa matawi na kuzaa matunda kwa ajili ya watu wangu wa Israeli, maana wao watarudi makwao karibuni.

9. Mimi niko upande wenu, nitahakikisha kuwa mnalimwa na kupandwa mbegu.

10. Waisraeli nitawazidisha sana. Miji itakaliwa, na magofu yatajengwa upya.

Kusoma sura kamili Ezekieli 36