Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 35:8-15 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Nitajaza milima yako watu waliouawa; na katika vilima vyako na mabonde yako na magenge yako yote watakuwako waliouawa kwa upanga.

9. Nitakufanya kuwa jangwa milele, na miji yako haitakaliwa tena. Ndipo utatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.

10. “Wewe ulisema ya kwamba mataifa hayo mawili yaani Yuda na Israeli ni mali yako na kwamba utazimiliki! Ulisema hivyo ingawa humo ni makao yangu mimi Mwenyezi-Mungu.

11. Kwa hiyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu naapa kwa nafsi yangu kwamba nitakutenda kadiri ya hasira na wivu wako, kulingana na chuki yako kwao. Nitakapokuadhibu utatambua mimi ni nani!

12. Wewe utajua ya kwamba mimi mwenyewe Mwenyezi-Mungu nimeyasikia matusi yote uliyoyatoa dhidi ya milima ya Israeli, ukisema: ‘Milima ya Israeli imefanywa kuwa jangwa! Tumepewa sisi tuinyakue!’

13. Nimesikia jinsi unavyojigamba na kusema maneno mengi dhidi yangu.

14. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitakapokufanya wewe Edomu kuwa jangwa, dunia yote itafurahi

15. kama wewe ulivyofanya wakati nchi ya Waisraeli ilipoharibiwa. Utakuwa jangwa, ewe mlima Seiri, pamoja na nchi yote ya Edomu. Ndipo watu watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”

Kusoma sura kamili Ezekieli 35