Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 32:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Siku ya kwanza ya mwezi wa kumi na mbili, mwaka wa kumi na mbili tangu uhamisho wetu, neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:

2. “Wewe mtu! Imba utenzi wa kuomboleza juu ya Farao, mfalme wa Misri.Wewe Farao unajiona kuwa simba kati ya mataifa,lakini wewe ni kama mamba tu majini:Unachomoka kwa nguvu kwenye mito yako,wayavuruga maji kwa miguu yako,na kuichafua mito.

3. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema:Nitautupa wavu wangu juu yako,nao watu watakuvua humo kwa wavu wangu.

4. Nitakutupa juu ya nchi kavu,nitakubwaga uwanjani,nitawafanya ndege wote watue juu yako,na kuwashibisha wanyama wote wa porini kwa mwili wako.

5. Nitatawanya nyama yako milimani,na kujaza mabonde yote mzoga wako.

6. Nchi nitainywesha damu yako mpaka milimani,mashimo yatajaa damu yako.

7. Nitakapokuangamiza, nitazifunika mbingu,nitazifanya nyota kuwa nyeusi,jua nitalifunika kwa mawingu,na mwezi hautatoa mwangaza wake.

Kusoma sura kamili Ezekieli 32