Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 31:5-13 Biblia Habari Njema (BHN)

5. “Kwa hiyo, ulirefuka sanakupita miti yote msituni;matawi yake yalizidi kuwa mengi na makubwa,kutokana na maji mengi mizizini mwake.

6. Ndege wote waliweka viota matawini mwake,chini yake wanyama walizaliwa,mataifa yote makubwa yaliburudika kivulini mwake.

7. Ulikuwa mzuri kwa ukubwa wake,na kwa urefu wa matawi yake.Mizizi yake ilipenya chinimpaka penye maji mengi.

8. Miongoni mwa mierezi ya bustanini mwa Mungu,hakuna mti uliolingana nao,wala misonobari haikulingana na matawi yake,mibambakofi haikuwa na matawi kama yake,hata mti wowote wa bustani ya Munguhaukulingana nao kwa uzuri.

9. Mimi niliufanya kuwa mzurikwa matawi yake mengi;ulionewa wivu na miti yote ya Edeniiliyokuwa katika bustani ya Mungu.

10. “Kwa hiyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Kwa sababu wewe ulirefusha kimo chake na kukiinua kilele chake kati ya matawi makubwa, ukajivunia urefu wake,

11. nitautia mikononi mwa mkuu kati ya mataifa. Yeye, atauadhibu. Nimeutupilia mbali kadiri ya uovu wake.

12. Watu wa mataifa mengine katili kupindukia, wataukata na kuubwaga chini na kuuacha. Matawi yake yataanguka chini mlimani na kila mahali mabondeni; yatavunjika na kutapakaa chini katika magenge yote. Watu wote wataondoka kivulini mwake na kuuacha.

13. Ndege wote watatua juu ya mabaki yake na wanyama wote wa porini watakanyaga matawi yake.

Kusoma sura kamili Ezekieli 31