Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 30:14-26 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Mji wa Pathrosi nitaufanya kuwa mtupu,mji wa Soani nitauwasha moto,mji wa Thebesi nitauadhibu.

15. Nitamwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu,ile ngome inayotegemewa na Misri;na kuangamiza makundi ya Thebesi.

16. Nitaiwasha moto nchi ya Misri.Pelusiumu utashikwa na dhiki kubwa,ukuta wa Thebesi utabomolewa,nao Memfisi utakabiliwa na adui mchana wazi.

17. Vijana wanaume wa Oni na Pi-besethi watauawa kwa upanga,na wakazi wengine watachukuliwa uhamishoni.

18. Huko Tahpanesi mchana utakuwa gizawakati nitavunja mamlaka ya Misrina kiburi chake kikuu kukomeshwa.Wingu litaifunika nchi ya Misrina watu wake watachukuliwa mateka.

19. Ndivyo nitakavyoiadhibu Misri.Na watu watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”

20. Siku ya saba ya mwezi wa kwanza, mwaka wa kumi na moja tangu uhamisho wetu, neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:

21. “Wewe mtu! Nimeuvunja mkono wa Farao mfalme wa Misri, nao haukufungwa ili uweze kupona na kuweza kushika upanga.

22. Kwa hiyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitapambana na Farao mfalme wa Misri. Nitaivunja mikono yake yote miwili, ule mzima na hata uliovunjika. Na upanga ulio mkononi mwake utaanguka chini.

23. Nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa na kuwasambaza katika nchi nyingine.

24. Mikono ya mfalme wa Babuloni nitaitia nguvu na kutia upanga wangu mkononi mwake. Lakini nitaivunja mikono ya Farao, naye atapiga kite mbele ya mfalme wa Babuloni kama mtu aliyejeruhiwa vibaya sana.

25. Mikono ya mfalme wa Babuloni nitaiimarisha, lakini mikono ya Farao italegea. Hapo watu watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu. Nitakapotia upanga wangu mkononi mwa mfalme wa Babuloni, ataunyosha dhidi ya nchi ya Misri,

26. nami nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa mengine na kuwasambaza katika nchi nyingine. Ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”

Kusoma sura kamili Ezekieli 30