Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 3:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Akaniambia, “Wewe mtu, kula unachopewa; kula kitabu hiki kisha uende ukawaeleze Waisraeli.”

2. Kwa hiyo nilifumbua kinywa changu, naye akanilisha hicho kitabu.

3. Halafu akaniambia, “Wewe mtu, kula kitabu hiki ninachokupa, ujaze tumbo lako.” Basi, nilikula kitabu hicho, nacho kikawa kitamu mdomoni kama asali.

4. Kisha akaniambia, “Wewe mtu, waendee Waisraeli, ukawaambie maneno yangu.

5. Sikutumi kwa taifa lenye lugha ngeni na ngumu, bali kwa Waisraeli.

6. Sikutumi kwa mataifa mengi yenye lugha ngeni na ngumu ambayo huifahamu. Kwani ningelikutuma kwa watu kama hao, hakika wao wangekusikiliza.

7. Lakini Waisraeli hawatakusikiliza, kwani hawana nia ya kunisikiliza mimi. Watu wote wa Israeli ni wenye kichwa kigumu na moyo mkaidi.

Kusoma sura kamili Ezekieli 3