Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 21:13-21 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Hilo litakuwa jaribio gumu sana.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

14. Wewe mtu, tabiri!Piga makofi,upanga na ufanye kazi yake,mara mbili, mara tatu.Huo ni upanga wa mauajinao unawazunguka.

15. Kwa hiyo wamekufa moyona wengi wanaanguka.Ncha ya upanga nimeiweka katika malango yao yote.Umefanywa ungae kama umeme,umengarishwa kwa ajili ya mauaji.

16. Ewe upanga, shambulia kulia, shambulia kushoto;elekeza ncha yako pande zote.

17. Nami nitapiga makofi,nitatosheleza ghadhabu yangu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

18. Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:

19. “Wewe mtu! Chora njia mbili ambapo utapitia upanga wa mfalme wa Babuloni. Njia zote mbili zianzie katika nchi moja. Mwanzoni mwa kila njia utaweka alama ya kuonesha upande mji uliko.

20. Utachora njia upanga utakapopitia kwenda kuufikilia mji wa Raba wa Waamoni, na njia nyingine inayoelekea mji wenye ngome wa Yerusalemu nchini Yuda.

21. Mfalme wa Babuloni anasimama mwanzoni mwa hizo njia mbili, kwenye njia panda, apate kupiga bao. Anatikisa mishale, anaviuliza shauri vinyago vya miungu yake na kuchunguza maini ya mnyama.

Kusoma sura kamili Ezekieli 21