Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 21:11-18 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Umenolewa na kungarishwauwekwe mkononi mwa mwuaji.

12. Wewe mtu, lia na kuombolezaupanga huo umenyoshwa dhidi ya watu wangu,dhidi ya wakuu wote wa Israeli.Wataangamizwa kwa upanga pamoja na watu wangu.Jipige kifua kwa huzuni.

13. Hilo litakuwa jaribio gumu sana.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

14. Wewe mtu, tabiri!Piga makofi,upanga na ufanye kazi yake,mara mbili, mara tatu.Huo ni upanga wa mauajinao unawazunguka.

15. Kwa hiyo wamekufa moyona wengi wanaanguka.Ncha ya upanga nimeiweka katika malango yao yote.Umefanywa ungae kama umeme,umengarishwa kwa ajili ya mauaji.

16. Ewe upanga, shambulia kulia, shambulia kushoto;elekeza ncha yako pande zote.

17. Nami nitapiga makofi,nitatosheleza ghadhabu yangu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

18. Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:

Kusoma sura kamili Ezekieli 21