Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 2:7-10 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Wewe utawaambia maneno yangu, hata kama watasikia au hawatasikia, maana wao ni watu waasi.

8. “Lakini ewe mtu, sikiliza ninayokuambia, wala usiwe mwasi kama watu hao. Fumbua kinywa chako, ule ninachokupa.”

9. Nilipotazama, niliona nimenyoshewa mkono, na kumbe ulikuwa na kitabu kilichoandikwa.

10. Basi akakifungua mbele yangu, nacho kilikuwa kimeandikwa mbele na nyuma maneno ya maombolezo, vilio na laana.

Kusoma sura kamili Ezekieli 2