Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 19:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mungu aliniambia niimbe utenzi huu wa maombolezo kuhusu wakuu wa Israeli:

2. Mama yenu alikuwa simba wa faharimiongoni mwa simba wengine.Alikaa kati ya simba vijana,akawalisha watoto wake.

3. Alimlea mtoto mmojawapo wa watoto wake,mtoto huyo naye akawa simba kijana hodari.Akajifunza kwa mama yake kuwinda,akawa simba mla watu.

4. Mataifa yakapiga mbiu ya hatari dhidi yake,wakamnasa katika mtego wao,wakampeleka kwa ndoana mpaka Misri.

5. Mama yake alipoona kuwa amechoka kungoja,matumaini ya kumpata yamekwisha,alimchukua mtoto wake mwingine,akamfanya simba kijana hodari.

6. Huyo alipokuwa amekua,akaanza kuzurura na simba wengine.Naye pia akajifunza kuwinda,akawa simba mla watu.

7. Aliziandama ngome za watuna kuiharibu miji yao.Nchi ikatishika pamoja na wakazi wake,kwa sauti ya kunguruma kwake.

8. Mataifa yakamkabili kutoka mkoani mwao kote,wakatandaza wavu wao juu yake,naye akanaswa katika mtego wao.

9. Kwa ndoana wakamtia katika kizimba chao,wakampeleka kwa mfalme wa Babuloni.Huko, wakamtia gerezani,ili ngurumo yake isisikike tenajuu ya milima ya Israeli.

Kusoma sura kamili Ezekieli 19