Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 17:9-12 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Sasa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nakuuliza:Je, mzabibu huo utaweza kustawi?Je, hawatangoa mizizi yakena kuozesha matunda yakena matawi yake machanga kuyanyausha?Hakutahitajika mtu mwenye nguvu au jeshikuungoa kutoka humo ardhini.

10. Umepandikizwa, lakini, je, utastawi?Upepo wa mashariki uvumapo juu yake utanyauka;utanyauka papo hapo kwenye kuta ulikoota.”

11. Kisha neno la Mwenyezi-Mungu likanijia:

12. “Sasa waulize hao watu waasi kama wanaelewa maana ya mfano huo. Waambie kuwa, mfalme wa Babuloni alikuja Yerusalemu, akamwondoa mfalme na viongozi wake, akawapeleka Babuloni.

Kusoma sura kamili Ezekieli 17