Agano la Kale

Agano Jipya

Danieli 8:14-25 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Yule mtakatifu wa kwanza akamjibu, ‘Kwa muda wa nyakati za jioni na asubuhi 2,300. Kisha maskani ya Mungu itapata tena hali yake halisi.’

15. “Mimi Danieli nilipoyaona hayo maono, na nilipokuwa nikijaribu kujua maana yake, ghafla, mmoja kama mwanaadamu akasimama mbele yangu.

16. Nikasikia sauti ya mwanaadamu kutoka katika mto Ulai ikiita, ‘Gabrieli, mweleze mtu huyu maana ya maono aliyoona.’

17. Gabrieli akaja karibu na mahali niliposimama. Mimi nikaogopa sana, hata nikaanguka kifudifudi. Lakini akaniambia, ‘Wewe mtu, elewa kwamba maono uliyoyaona yanahusu wakati wa mwisho.’

18. “Alipokuwa anazungumza nami, mimi nikashikwa na usingizi mzito huku nimelala kifudifudi. Lakini yeye akanishika na kunisimamisha.

19. Kisha akaniambia, ‘Sikiliza, ninakufahamisha matokeo ya ghadhabu ya Mungu yatakavyokuwa. Maono hayo yanahusu wakati wa mwisho.

20. “ ‘Yule kondoo dume uliyemwona mwenye pembe mbili, ni wafalme wa Media na Persia.

21. Yule beberu ni mfalme wa Ugiriki. Ile pembe kubwa katikati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.

22. Ile pembe iliyovunjika na badala yake zikaota pembe nne, ina maana kwamba ufalme huo mmoja utagawanyika kuwa falme nne, lakini falme hizo hazitakuwa na nguvu kama ule ufalme wa kwanza.

23. Wakati falme hizo zitakapofikia kikomo chake na uovu wao kufikia kilele chake, patatokea mfalme mmoja shupavu na mwerevu.

24. Atakuwa mwenye mamlaka makubwa, atasababisha uharibifu mbaya sana, na atafanikiwa katika kila atendalo. Atawaangamiza watu maarufu na watakatifu wa Mungu.

25. Kwa ujanja wake, atafanikiwa katika mipango yake ya hila, naye atajikweza. Atawaangamiza watu wengi bila taarifa, na atataka kupigana na Mkuu wa wakuu, lakini ataangamizwa pasipo kutumia nguvu za kibinadamu.

Kusoma sura kamili Danieli 8