Agano la Kale

Agano Jipya

Amosi 5:20-27 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Siku ya Mwenyezi-Mungu itakuwa giza, na sio mwanga;itakuwa huzuni bila uangavu wowote.

21. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nazichukia na kuzidharau sikukuu zenu;siifurahii mikutano yenu ya kidini.

22. Mjaponitolea sadaka zenu za kuteketezwa na za nafaka,mimi sitakubali kuzipokea;na sadaka zenu za amani za wanyama wanonomimi sitaziangalia kabisa.

23. Ondoeni mbele yangu kelele za nyimbo zenu!Sitaki kusikiliza muziki wa vinubi vyenu!

24. Lakini acheni haki itiririke kama maji,uadilifu uwe kama mto usiokauka.

25. “Enyi Waisraeli, wakati ule mlipokuwa kule jangwani kwa miaka arubaini, je, mliniletea tambiko na sadaka hata mara moja?

26. Je, wakati huo mlibeba kama sasa vinyago vya mungu wenu Sakuthi mfalme wenu na vinyago vya Kaiwani mungu wenu wa nyota, vitu ambavyo mlijitengenezea wenyewe?

27. Kwa hiyo nitawapeleka uhamishoni, mbali kuliko Damasko! Hayo amesema Mwenyezi-Mungu, ambaye jina lake ni Mungu wa Majeshi.

Kusoma sura kamili Amosi 5