Agano la Kale

Agano Jipya

2 Wafalme 5:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Naamani, kamanda wa jeshi la mfalme wa Aramu alikuwa mtu mashuhuri aliyependwa sana na bwana wake, kwani kwa njia yake Mwenyezi-Mungu aliiletea nchi ya Aramu ushindi. Alikuwa askari hodari, lakini alikuwa na ugonjwa wa ukoma.

2. Katika vita walivyokuwa wakipigana na Israeli, Waaramu walikuwa wamemchukua msichana mmoja mdogo kutoka Israeli, naye akawa anamtumikia mke wa Naamani.

3. Siku moja akamwambia bibi yake, mke wa Naamani, “Laiti bwana wangu angekwenda na kumwona yule nabii aliyeko Samaria! Angemponya ugonjwa wake.”

4. Naamani alipopata habari hizi, akaenda kwa mfalme na kumweleza habari za mtoto huyu.

5. Mfalme wa Aramu akamwambia, “Chukua barua hii umpelekee mfalme wa Israeli.”Hivyo Naamani akaondoka, huku amechukua vipande 30,000 vya fedha, vipande 6,000 vya dhahabu na mavazi kumi ya sikukuu.

Kusoma sura kamili 2 Wafalme 5