24. Asaheli, nduguye Yoabu, alikuwa mmoja wa mashujaa thelathini. Mashujaa wengine wa Daudi walikuwa: Elhanani, mwana wa Dodo wa Bethlehemu;
25. Shama, Mharodi; Elika, Mharodi;
26. Helesi, Mpalti; Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoa;
27. Abiezeri, Mwanathothi; Mebunai, Mhushathi;
28. Salmoni, Mwahohi; Maharai, Mnetofathi;
29. Helebu mwana wa Baana, Mnetofathi; Itai mwana wa Ribai, toka Gibea katika Benyamini;
30. Benaya, Mpirathoni; Hidai, wa vijito vya Gaashi;
31. Abialboni, Mwarbathi; Azmawethi, Mbahurimu;
32. Eliaba, Mshaalboni; wana wa Yasheni; Yonathani;
33. Shama, Mharari; Ahimu mwana wa Sharari, Mharari;
34. Elifeleti mwana wa Ahasbai, Mmaaka; Eliamu mwana wa Ahithofeli, Mgiloni;
35. Hesrawi, Mkarmeli; Paarai, Mwarbi;
36. Igali mwana wa Nathani, Msoba; Bani, Mgadi;
37. Seleki, Mwamoni; Naharai, Mbeerothi aliyekuwa mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya;
38. Ira na Garebu, Waithri;