Agano la Kale

Agano Jipya

2 Samueli 1:24-27 Biblia Habari Njema (BHN)

24. “Wanawake wa Israeli, mlilieni Shauli!Aliwavika mavazi mekundu ya fahari,aliyatarizi mavazi yenu kwa dhahabu.

25. “Jinsi gani mashujaa walivyoanguka!Wamekufa wakiwa katika mapambano.Yonathani analala,akiwa ameuawa milimani.

26. Nasikitika kwa ajili yako, ndugu yangu Yonathani.Umekuwa kwangu daima mtu wa kupendeza,pendo lako kwangu limekuwa la ajabu,la ajabu kuliko la mwanamke.

27. “Jinsi gani mashujaa wameanguka,na silaha zao zimeachwa, hazina kazi.”

Kusoma sura kamili 2 Samueli 1