Agano la Kale

Agano Jipya

2 Mambo Ya Nyakati 9:25-30 Biblia Habari Njema (BHN)

25. Mfalme Solomoni akawa na vibanda 4,000 vya kuwekea farasi na magari, na askari wapandafarasi 12,000 ambao aliwaweka katika miji yenye vituo vya magari ya farasi na katika Yerusalemu.

26. Aliwatawala wafalme wote waliokuwako kuanzia mto Eufrate, hadi nchi ya Wafilisti na hadi mpakani na Misri.

27. Basi Solomoni alifanya fedha katika Yerusalemu kuwa kitu cha kawaida kama mawe katika Yerusalemu, na mbao za mierezi zilipatikana kwa wingi kama mikuyu iliyomo Shefela.

28. Solomoni aliletewa farasi walionunuliwa kutoka Misri na nchi nyinginezo.

29. Matendo mengine ya Solomoni, kutoka mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha “Historia ya Nabii Nathani,” katika “Unabii wa Ahiya wa Shilo,” na katika “Maono ya Ido” mwonaji, ambayo yahusu pia Yeroboamu mwana wa Nebati.

30. Solomoni alitawala nchi yote ya Israeli kwa miaka arubaini.

Kusoma sura kamili 2 Mambo Ya Nyakati 9