Agano la Kale

Agano Jipya

2 Mambo Ya Nyakati 8:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Miaka ishirini, ambayo Solomoni aliijenga nyumba ya Mwenyezi-Mungu na ikulu ilipokwisha kupita,

2. Solomoni aliijenga upya miji aliyopewa na Huramu, halafu akawapa Waisraeli miji hiyo waishi humo.

3. Baadaye Solomoni alielekea Hamath-zoba na kuuteka,

4. na kuujenga mji wa Tadmori nyikani. Aliijenga upya miji ya ghala iliyokuwa huko Hamathi.

5. Kadhalika, Solomoni alijenga miji ifuatayo: Beth-horoni wa juu, na Beth-horoni wa chini, miji yenye ngome, kuta, malango na makomeo,

Kusoma sura kamili 2 Mambo Ya Nyakati 8