Agano la Kale

Agano Jipya

2 Mambo Ya Nyakati 6:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ndipo Solomoni akasema,“Mwenyezi-Mungu alisema ya kwambaatakaa katika giza nene.

2. Hakika nimekujengea nyumba tukufu,mahali pa makao yako ya milele.”

3. Kisha Solomoni akaigeukia jumuiya yote ya watu wa Israeli wakiwa wamesimama, akawabariki.

4. Akasema, “Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kwani kwa nguvu yake ameitimiza ahadi yake aliyoitoa kwa baba yangu Daudi akisema,

5. ‘Tangu niwaondoe watu wangu kutoka nchi ya Misri, sikuchagua mji wowote katika makabila ya Israeli ili nijengewe nyumba nitakamoabudiwa; na sikumchagua mtu yeyote awe mkuu wa watu wangu Israeli.

Kusoma sura kamili 2 Mambo Ya Nyakati 6