Agano la Kale

Agano Jipya

2 Mambo Ya Nyakati 35:20-27 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Baada ya haya yote aliyofanya mfalme Yosia kwa ajili ya hekalu, Neko, mfalme wa Misri, aliongoza jeshi lake kwenda kushambulia Karkemishi kwenye mto Eufrate. Naye mfalme Yosia alitoka kumkabili,

21. lakini mfalme Neko akamtumia ujumbe usemao: “Vita hivi havikuhusu wewe hata kidogo ewe mfalme wa Yuda. Sikuja kupigana nawe bali dhidi ya maadui zangu, na Mungu ameniamuru niharakishe. Acha basi kumpinga Mungu, ambaye yu upande wangu, la sivyo atakuangamiza.”

22. Lakini Yosia hakukubali kumwachia. Alikataa kuyasikiliza maneno aliyonena Mungu kwa njia ya Neko, kwa hiyo akajibadilisha ili asitambulike, kisha akaingia vitani katika tambarare ya Megido.

23. Nao wapiga upinde walimpiga mshale mfalme Yosia; basi ndipo mfalme alipowaambia watumishi wake: “Niondoeni! Nimejeruhiwa vibaya sana.”

24. Watumishi wake walimtoa katika gari lake la farasi, wakambeba na gari lake la pili hadi Yerusalemu. Hapo akafariki dunia na kuzikwa katika makaburi ya kifalme. Watu wote wa Yuda na Yerusalemu waliomboleza kifo cha Yosia.

25. Nabii Yeremia pia alitunga shairi la maombolezo kwa ajili ya kifo chake; nao waimbaji wote, wanaume kwa wanawake, humtaja Yosia katika maombolezo yao, mpaka leo. Imekuwa desturi kufanya maombolezo haya katika Israeli. Hayo yameandikwa katika Maombolezo.

26. Matendo mengine ya Yosia na matendo yake mema kama yalivyoandikwa katika sheria ya Mwenyezi-Mungu,

27. na matendo yake tangu mwanzo hadi mwisho, hayo yameandikwa katika Kitabu cha Wafalme wa Israeli na Yuda.

Kusoma sura kamili 2 Mambo Ya Nyakati 35