Agano la Kale

Agano Jipya

2 Mambo Ya Nyakati 29:13-18 Biblia Habari Njema (BHN)

13. ukoo wa Elisafani: Shimori na Yeneli,

14. ukoo wa Hemani: Zekaria na Matania; ukoo wa Yeduthuni: Shemaya na Uzieli.

15. Hawa waliwakusanya Walawi wenzao, wakajitakasa. Kisha wakaingia kama walivyotakiwa kufanya na mfalme, wakaanza kusafisha nyumba ya Mwenyezi-Mungu kama Mwenyezi-Mungu alivyoagiza.

16. Makuhani waliingia katika sehemu ya ndani ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakautoa uchafu wote uliokuwemo, wakauweka uani. Kutoka hapo, Walawi waliuchukua uchafu huo mpaka nje kwenye Bonde la Kidroni.

17. Walianza kazi ya kulitakasa hekalu siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, na kufikia siku ya nane, wakawa wamekwisha maliza kazi yote, hata na ukumbini. Kisha, walifanya kazi kwa muda wa siku nane zaidi hadi siku ya kumi na sita ya mwezi huo, kila kitu kilikamilika.

18. Baadaye, Walawi walimwendea mfalme Hezekia wakamwambia, “Tumekwisha litakasa hekalu lote pamoja na madhabahu ya tambiko za kuteketeza na vyombo vyake vyote, na meza ya mikate mitakatifu na vyombo vyake vyote.

Kusoma sura kamili 2 Mambo Ya Nyakati 29