Agano la Kale

Agano Jipya

2 Mambo Ya Nyakati 27:5-9 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Alipigana vita dhidi ya mfalme wa Amoni na kuwashinda. Katika mwaka huo Waamoni walimtolea ushuru wa kilo 3,400, tani 1,000 za ngano na kilo 1,000 za shayiri; waliendelea kufanya hivyo katika mwaka wa pili na wa tatu.

6. Mfalme Yothamu aliendelea kuwa mwenye nguvu, kwa sababu aliishi kwa kumtii Mwenyezi-Mungu, Mungu wake.

7. Matendo mengine ya Yothamu, vita vyake na maongozi yake, yote yameandikwa katika Kitabu cha Habari za Wafalme wa Israeli na Yuda.

8. Yothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, akatawala kwa muda wa miaka kumi na sita huko Yerusalemu.

9. Alifariki na kuzikwa katika mji wa Daudi. Naye Ahazi mwanawe akatawala mahali pake.

Kusoma sura kamili 2 Mambo Ya Nyakati 27