Agano la Kale

Agano Jipya

2 Mambo Ya Nyakati 27:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Yothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita huko Yerusalemu. Mama yake aliitwa Yerusha binti Sadoki.

2. Alitenda mema mbele ya Mwenyezi-Mungu kama alivyofanya Uzia baba yake; isipokuwa yeye hakuingia katika hekalu la Mwenyezi-Mungu nao watu waliendelea kufanya maovu.

3. Yothamu alijenga Lango la Kaskazini la nyumba ya Mwenyezi-Mungu na kushughulika sana na ujenzi wa ukuta sehemu ya Ofeli.

4. Alijenga miji kwenye nchi ya milima ya Yuda, na kwenye misitu, akajenga ngome na minara katika milima yenye misitu.

5. Alipigana vita dhidi ya mfalme wa Amoni na kuwashinda. Katika mwaka huo Waamoni walimtolea ushuru wa kilo 3,400, tani 1,000 za ngano na kilo 1,000 za shayiri; waliendelea kufanya hivyo katika mwaka wa pili na wa tatu.

6. Mfalme Yothamu aliendelea kuwa mwenye nguvu, kwa sababu aliishi kwa kumtii Mwenyezi-Mungu, Mungu wake.

Kusoma sura kamili 2 Mambo Ya Nyakati 27