Agano la Kale

Agano Jipya

2 Mambo Ya Nyakati 26:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha watu wote wa Yuda wakamchukua Uzia mwanawe Amazia akiwa mwenye umri wa miaka kumi na sita, wakamtawaza mahali pa Amazia baba yake.

2. Halafu baada ya kifo cha baba yake aliujenga upya mji wa Elothi na kuurudisha kwa Yuda.

3. Uzia alianza kutawala akiwa na umri wa miaka kumi na sita; akatawala kwa muda wa miaka hamsini na miwili huko Yerusalemu. Mama yake alikuwa Yekolia wa Yerusalemu.

4. Alitenda mema mbele ya Mwenyezi-Mungu kama baba yake.

5. Alimtumikia Mwenyezi-Mungu kwa uaminifu wakati wa kuishi kwa Zekaria, aliyemfundisha kumtii Mungu. Kadiri alivyomtafuta Mungu, Mungu alimfanikisha.

6. Uzia aliondoka akapiga vita dhidi ya Wafilisti, akazibomoa kuta za miji ya Gathi, Yabne na Ashdodi. Akajenga miji katika eneo la Ashdodi na kwingineko nchini Filistia.

7. Mungu alimsaidia kuwashinda Wafilisti, Waarabu waliokaa Gurbaali na Wameuni.

8. Waamoni walimlipa kodi, na sifa zake zikaenea hadi Misri, kwa sababu alipata nguvu.

9. Tena Uzia alijenga minara katika Yerusalemu penye Lango la Pembeni, Lango la Bondeni na Pembeni na kuiimarisha.

Kusoma sura kamili 2 Mambo Ya Nyakati 26